Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Msanii Tunda Man Ataja Sababu Za Wasanii Waliooa Kupotea Kwenye Muziki

Msanii wa muziki Tunda Man amefunguka kwa kueleza kwanini baadhi ya wasaani wa muziki wakioa wanapotea kwenye muziki.

Tunda ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wengi wanapotea kwenye muziki kutokana na kutoa nyimbo ambazo zinawazungumzia wake zao.
“Msanii akioa eti anapotea kwenye muziki hizo ni dhana potofu, kuna wasanii wengi wameoa na bado wanafanya vizuri, wapo akina Mr Blue wanafanya vizuri,” Tunda aliimbia Bongo5 “Mimi najua msanii anaweza kupotea kama anatoa nyimbo za kumuimbia mke wake, mke wako unatakiwa kumuimbia ndani mwako, na jamii inataka muziki wao,”
Muimbaji huyo aliingia kwenye maisha ya ndoa mapema mwaka jana.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017