Pamoja
na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa
sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.
Kwa kiasi
kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni
wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi
tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za
Ndoa na Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache
ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko.
(Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa
kabisa)
Vigezo vilivyopitiliza
viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini
unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye
angependa awe mume wake.Wanawake hawa
hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa
kumuoa awe nazo.
Vigezo hivyo huwa hata
kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume
huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati,
sauti nzuri n.k.
Inaweza kuwa kama
mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao
anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile
ambavyo yeye anataka mumewe awe.
Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa
hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo tayari
kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume
ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai
hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari.
Hivyo hukazana
kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa,
bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
Kutompata Mwanaume
Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani
na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini
anakupenda pia.
Wengi katika kundi
hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine
hufuata kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo
vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye kikubwa
anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa
huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke anaamini
msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka
hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.
Kuchagua mno Wanaume
wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama
kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa
aina ipi wanataka.
Akija wa mwenye uwezo
atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama
kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo.
Akija wa kabila hii,
atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani
kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka
kumuoa.
Hatimaye inaweza
tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa
hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.
Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia
uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa
waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani.
Hata hivyo hapo
hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona
ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi
hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu
anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana.
Kitendo hiki hukuza
nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba
wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau
na kiburi.
Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka
18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana
mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani
sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.
Katika kundi
hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na
bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni
mkubwa na anafaa kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale
ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na
umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni
kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na
wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa
na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana
wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama
kuwahi kuwa na mtoto.
Wengi sana
hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa
tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni
waathirika; afya hudhoofika zaidi.
Kutaka maisha ya
Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha
maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka
hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo linafanya vigezo
ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza
yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi hushindwa
kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo
yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi
kiachwe kama kilivyo.
Kuona taasisi ya Ndoa
kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu,
huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina
ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki,
majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia
ndoa mbovu: Hii
inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe
(pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila
ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha
ya taabu na kuonewa.
- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya
lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume
kwake anaona kama ni utumwa.
Kutokuwa kabisa na
mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana
hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama
kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni
waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu
baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa
mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini