Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

ROMA Awa Mwalimu wa Hisabati, Mcheki Akikata Namba Darasani

Rapa namba moja kwa mwenye hits song zenye kudumu miaka dahali, Ibrahimu Musa ‘Roma Mkatoriki’, June 15 mwaka huu alirudi kwa muda kwenye taaaluma yake ya ualimu na kufundisha somo la hisabati darasa la saba katika shule ya msingi Mchikichini iliyopo Mbagala rangi tatu.
Akizungumza mbele ya kamera ya Gazeti hili Roma amesema, uamuzi wa kwenda kufundisha shuleni hapo umekuja baada ya kuona kuona hamasa juu ya wanafunzi kupenda a somo la hisabati katika shule mbalimbali nchini imeporomoka kwa kiasi kukubwa.

Roma akiwa darasani anafundisha somo la hisabati.
“Nimekwenda kufundisha katika shule hiyo kwa mantiki ya jambo moja kubwa, kutoa hamasa kwa wanafunzi wa shule mbalimbali nchini kupenda masomo ya hisabati, somo ambalo limekuwa likiogopwa na wanafunzi wengi nchini, nimeamua kuchagua shule ya Mchikichini kwakuwa ni shule ya serikali inayokabiliwa na changamoto nyingi za miundombinu na taaluma” alisema Roma.
Sambamba na hayo, Mwanamuziki huyo ambaye aliandamana na mkewe katika shule hiyo, alitoa zawadi ya vitabu vya hisabati kwa darasa la saba mbele ya mwalimu mkuu Melkiol Kamagi ambaye amemshukuru Roma na kutoa wito kwa wasanii wengine kuwa na moyo kama wa Rapa huyo kuisaidia jamii katika mambo mbalimbali.
“Kwanza kabisa nimshukuru Roma Mkatoriki kwa kuja kututembelea ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wanafunzi na kuwafundisha, lakini kubwa zaidi ni kutuachia zawadi ya vitabu vya hisabati katika shule yetu, msaada huu umekuja wakati muafaka kwani shule ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa vitabu, pia nitoe wito kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kuisaidia jamii yao kama hivi” alisema mkuu wa shule hiyo.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017