Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Serikali Yakamilisha Upelelezi Kesi Ya Masogange, Yapeleka Mashahidi


Serikali imekamilisha Upelelezi wa Kesi ya Dawa za Kulevya inayomkabili Video Queen Agnes Gerald (28) maarufu kama Masogange.

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza kesi  hiyo Julai 13, mwaka huu

Hatua hiyo imekija baada upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi na leo kumsomea mshtakwa maelezo ya awali (PH).

Katika (PH) Hiyo Masogange amekiri kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kuchukuliwa sampuli ya mkojo wake ili kuthibitisha kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange amekubali hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alipokuwa akimsomea maelezo ya awali ya mashitaka yake.

Pia Masogange amekiri kuwa Februari 14, mwaka huu alikamatwa nyumbani kwake Makongo juu Kinondoni Dar es Salaam na kupelekwa Kituo cha Polisi Central

Ikadaiwa kuwa, Februari 15, mwaka huu Masogange alipelekwa kwa mkemia kuchukuliwa sampuli zake.Aidha, alikiri kuwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 783597.

Hata hivyo, Mshitakiwa huyo amekana kuwa Februari 20, mwaka huu Mkemia Mkuu alitoa taarifa iliyothibitisha kwamba mkojo wake ulikuwa na dawa aina ya heroin na Oxazepam.

Kufuatia hayo, kesi hiyo itaendelea Julai 13 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utaleta mashahidi wake.

Masogange anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Inadaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.

Aidha anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Masogange yupo nje kwa dhamana.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017