Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Uwoya Amfanyia Kitu Kibaya Mdogo wa Zari

Irene Uwoya
MADAI mazito! Staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya, anatuhumiwa kumfanyia fujo mdogo wa mjasiriamali maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aliyetajwa kwa jina moja la Asmah, Wikienda  lina ubuyu ulionyooka.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lililofunga mtaa lilijri nyumbani kwa mwanaume aliyetambulika kwa jina la Patrick Christopher ‘PCK’.
Mdogo wa Zari Asmah

Chanzo hicho makini kililieleza Wikienda kuwa, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni nyumbani kwa jamaa huyo, maeneo ya Msasani jijini Dar, majira ya saa 1:00 usiku ambapo mwanaume huyo ambaye ni bwana wa video queen maarufu Bongo aitwaye Bhoke Wambura ‘Kibonge Sexy’ ambaye yupo safarini nje ya nchi, aliingia nyumbani kwake hapo akiwa na mrembo huyo.


Patrick Christopher ‘PCK’.
“Baada ya PCK kuingia ndani kwake akiwa na Asmah aliyekuwa akitokea kwao nchini Uganda, Uwoya na timu yake nao walifika na kuanza kufanya fujo huku wakirusha mawe ndani ya nyumba hiyo na kuzua tafrani ya ajabu iliyosababisha mtaa kufungwa,” kilisema chanzo ambacho ni shuhuda namba moja aliyekuwa eneo hilo la tukio.

Baada ya kupata habari hizo, Wikienda lilimtafuta PCK ambaye alikiri kuwa na Asmah na kufanyiwa fujo nyumbani kwake na Uwoya.

Alisema kuwa, wakati anapatwa na tukio hilo alikuwa akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar, kumpokea mpenzi wake huyo aliyetoka Uganda ambapo tukio hilo waliliweka live kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na huko ndiko Uwoya alipopata habari.


“Ni kweli Uwoya amewahi kuwa mpenzi wangu na tulipoachana aliniapia kwamba atakuwa ananiharibia kwa kila mwanamke nitakayekuwa naye hivyo siku hiyo baada ya kuingia tu na mpenzi wangu huyu ambaye ni mdogo wake Zari yaani Asmah ndipo fujo zikaanza.

“Akiwa na timu yake, Uwoya alirusha mawe na kufanya fujo za kutosha hapa nyumbani kwangu, hata kamera zangu za CCTV zinaonesha tukio zima lilivyokuwa, sijui huyu mwanamke anataka nini kwangu kwa kweli,” alisema PCK.

UWOYA ANASEMAJE?
Baada ya kupata ishu kutoka kwa sosi na jamaa huyo, Wikienda lilimgeukia Uwoya ili kusikia upande wake ambapo alisikiliza tuhuma zote kasha akacheka na kusema:

“Siyo kweli na sipo kabisa Bongo niko Nairobi (Kenya), mwambieni huyo jamaa aachane na mimi nitamfunga.”
Hvi karibuni, Uwoya aliripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Risasi Jumamosi kuwa kwenye ugomvi na Kibonge Sexy, kisa kikielezwa ni huyohuyo mwanaume ambaye ilisemekana kuwa wanamgombea.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017