DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Salome Makamba amehoji bungeni sababu zilizoifanya serikali kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato, ambako ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kuacha kufanya hivyo kwenye maeneo mengine mengi yenye fursa za kiuchumi.
Mhe. Salome ameyasema hayo bungeni wakati akichangia kwenye bajeti ya mwaka huu ambapo amesema sababu kubwa ya kushindwa kutekeleza kwa bajeti iliyopita, ni kwa sababu ya serikali kushindwa kusimamia mambo ya msingi.
Mbunge huyo ameenda mbele na kutaka kujua ni utaratibu gani umetumika kusimamia gharama za ujenzi wa uwanja huo, sambamba na kutaka kujua kuhusu ununuzi wa ndege uliofanywa na serikali.
Akataka ufafanuzi pia utolewe kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es Salaam.
VIDEO: MSIKILIZE AKIHOJI BUNGENI
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini