Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Video: Penati Zilizoitupa Simba Nje Ya Sportpesa Super Cup

Kama hukuona mikwaju ya penati iliyoamua hatma ya Simba kwenye michuano ya SportPesa Super Cup, Daud TV ilinasa matuta yaliyoitupa Simba nje ya mashindano hayo.
Simba ilikalishwa kwa kufungwa penati 5-4 na timu ya Nakuru All Stars ya Kenya baada ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 90 za mchezo.
Wachezaji wa Simba waliofunga mikwaju yao ya penati ni Janvier Besala Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa na Fiston Munezero huku golikipa wao Daniel Agyei mkwaju wake wa penati ukipaa juu.
Penati za Nakuru zilifungwa na Baraka Nturukundo, Aman Kyata, Maina Kangethe, Amakanji Ekmba na Kamau Nganga.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017