Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Vyakula Vya Kuepuka Kuanza Kula Wakati Wa Kufuturu


Kufuturu ni jambo linalofanywa kila siku na waumini wa dini ya kiislamu wanaofunga katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Lakini kiuhalisia kufuturu au kula chakula baada ya mfungo wa siku nzima, ni jambo linaloweza kufanywa na yeyote, na si lazima iwe kipindi cha mfungo. Baadhi, kama wakristo hufunga wakati wowote mtu anapotaka kwa ajili ya maombi yake.
Lakini wakati wa kufuturu, si vyakula vyote unashauriwa kuanza kuvila wakati tumboni mwako hamn kitu. Kuna baadhi ya vyakula hutakiwi kuvila kwanza, na hapa chini tutaelezea baadhi.
Juisi ya matunda yenye kiwango kingi cha sukari
Juisi zenye kiwango kikubwa cha sukari haushauri kuzitumia mara tu unapofuturu kwani inaongeza kiwango kikubwa cha sukari ndani ya mwili wako ambayo kwa wakati huo hauitumii.
Lakini pia ukianza kula chakula chenye sukari nyingi mbali na kuongeza kiasi cha sukari mwili kutakufanya ujisikie kushiba kwa muda mfupi, ambapo kama kesho yake utafunga tena njaa huenda ikakusumbua.
Kawaha au Chai
Najua hii ndio hutumiwa na watu walio wengi sana ambao husema wanapasha tumbo joto baada ya mfungo ndipo waweze kula kitu kingine. Kunywa caffeine ambayo hupatikana kwenye kahawa au chai wakati tumbo lako halina kitu huweza kukuletea matatizo ya tumbo yanayoweza kukupelekea kutapika
Amira
Ulaji wa baadhi ya vyakula venye amira mfano donati au ‘pastry’ za nyama huwa na amira ambayo huweza kukusababishia kuvimbiwa au kulifanya tumbo lako lisiwe sawa. Mbali na tumbo kutokuwa sawa pia inaweza kukupelekea kutoa ushuzi mara kwa mara.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017