Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Watoto Waliopata Ajali Arusha Wapata Dili Kubwa Marekani Sasa Kupeperusha Bendera Ya Taifa

WATOTO Sadia, Wilson na Doreen kesho Jumamosi, Juni 10 wanatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakiwa kama waamuzi, au marefa wa heshima “Honorary Referees” kwenye mechi ya mpira wa miguu (American Football) utakaochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Tyson Arena mjini Sioux City kuanzia saa 2 usiku (saa za CST-Sioux City IA). 
Mashabiki zaidi ya 4,000 wanatarajiwa kuwepo uwanjani kuishabikia timu ya mji wa Sioux iitwayo “Sioux Bandits” ikichuana na timu ngeni.
(Picha kutoka Tyson Arena, Sioux City WATOTO Wilson na Sadia, Dkt Mashalla, Mama Wilson kwa pamoja wakiwa na baadhi ya wachezaji wa Sioux Bandits Jana wakijiandaa na shughuli ya kesho) MTOTO Doreen alitakiwa kupumzika zaidi siku ya Jana na Leo kwa Ratiba ya Madaktari

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017