Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Diamond aeleza biashara inayomlipa zaidi kati ya ‘Chibu Perfume Vs Karanga’


Inafahamika kuwa msanii wa muziki Bongo Flava, Diamond Platnumz miongoni mwa biashara anazomiliki ni Chibu Perfume na Diamond Karanga, sasa ametaja ipi inamlipa kati ya hizi mbili.
Hivi karibuni akiwa katika media tour nchini Uingereza aliulizwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ni biashara ipi inamlipa zaidi na jibu lake lake lilikuwa; ‘Off course, Diamond Karanga’.

Katika hatua nyingine alizungumzia kinachomsukuma zaidi kufungua biashara mbali mbali kwa kusema kuwa anataka kutumia muziki wake katika njia ya kujinufaisha hata pale atakapoacha muziki.

Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa

“Unaweza kuwa mwanamuziki lakini ukaweza kufanya vitu vingine katika misingi bora ukatengeneza ajira kwa wenzako ukatengeneza kitu ambacho hata kesho na kesho kutwa usipoweza kuimba ukaweza kupata riziki na familia yako ikanufaika” amesema Diamond.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017