BAADA ya straika wa
Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba
katika Ligi Kuu Bara, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, amesema tuzo hiyo
imefika sehemu iliyostahili.
Chirwa ambaye
aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba
Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, katika
kuwania tuzo hiyo, amewashinda Erasto Nyoni wa Simba na Ibrahim Ajibu wa Yanga.
Niyonzima alisema hafahamu
vinatumika vigezo gani kumpata mshindi wa tuzo hizo, lakini Chirwa anafaa kuwa
mshindi kwa mwezi huo kwani hata katika mechi dhidi yao alionyesha kiwango
kizuri.
“Chirwa kupewa
uchezaji bora wa mwezi hajapendelewa bali amestahili kwani nimemuona katika
mchezo waliocheza dhidi ya Stand United kule Shinyanga alipambana sana pamoja
na kufunga bao moja.
“Utaona hadi
siku hiyo Yanga inaibuka kwa ushindi wa mabao manne mchango wake ulikuwa mkubwa
sana pia hata kwenye ‘derby’ yetu aliisaidia sana Yanga,” alisema Niyonzima.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini