Hospital ya Aga Khan wameanza kurudisha matiti kwa wakina Mama waliokatwa kutokana na Magonjwa ya Kansa na waliopata majanga mbalimbali hata yale ya ukatili na kuungua moto ambapo siku ya leo wataanza na mgonjwa mmoja.
Akizungumza na waandishi leo hii Jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji katika hospital hiyo Dr. Aidan Njau amesema wanawake wenye matatizo kama hayo wamekua wakipata maumivu makali ambapo pia wamekua wakijisikia vibaya kwenye jamii.
“Tunaanza kutengeneza kwa wanawake waliokatwa matiti tutao nyama hiyo kwenye sehemu yake ya mwili na kubandika kwenye sehemu aliyokatwa ambapo muonekano wake utarudi kama alivyokuwa” Amesema.
Amesema Tanzania itashuhudia Wanawake wakipandikizwa matiti jambo ambalo halijawahi kutokea hivyo wanawake wenye tatizo hilo wajitokeze hospitalini hapo na waweze kupatiwa huduma hiyo.
Aidha upasuaji huo utafanywa na madaktari wawili akiwemo yeye na Daktari bingwa Edwin Mrema kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo amesema wanataka kurudisha furaha kwa wanamam wenye matatizo .
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini