Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Je Ni Kweli NGOMA Anakwenda Singida United? Ukweli Huu Hapa


Baada ya kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari  kuwa Uongozi wa Yanga na Singida United huenda ukabadilishana wachezaji wakati wa dirisha dogo kwa Donald Ngoma kwenda Singida United na Kutinyu mchezaji wa kimataifa naye kutoka Zimbabwe kama ilivyo kwa Ngoma kutua Yanga Uongozi wa Yanga msomaji wa Kwataunit.com  umelitolea ufafanuzi suala hilo.

Afisa habari makini Dismas Ten ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano katika klabu ya Yanga amesema wao kama uongozi wa Yanga hawajatoa taarifa yoyote na hawajazungumza na Singida United.
>>KUSOMA HABARI NYINGI ZA MICHEZO BOFYA HAPA<<


Huwezi kuwazungumzia watu kuzungumza lakini sisi kama klabu hatujatoa taarifa kuhusiana na jambo hilo na hakuna mazungumzo yoyote na Singida United kuhusiana na suala hilo.

Kuhusu kama Yanga wako tayari kufanya ubadilishano huo msomaji wa Kwataunit.com Dismas Ten amesema
Hilo ni suala la Upande mwingine, siyo suala geni kwenye mpira wa Miguu mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine ni suala ambalo lipo toka mpira wa miguu umeanzishwa kikubwa ni kufuata utaratibu na kuangalia maslahi ya pande zote klabu na wachezaji husika kwahiyo suala linajadiliwa kwa taratibu husika.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017