
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa na beki kisiki, Mtogo, Vincent Bossou (kushoto).
IMEBAINIKA kuwa benchi la ufundi la Yanga lipo kwenye mchakato mkubwa wa kumrejesha aliyekuwa beki wao kisiki, Mtogo, Vincent Bossou kwenye usajili wa dirisha dogo ambapo tayari hivi karibuni mmoja wa viongozi alitumwa nchini Togo alipo mchezaji huyo kwa ajili ya kuongea naye ili waingie mkataba.
Yanga iliachana na Bossou mwanzoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa miaka miwili kufika ukingoni ambapo tangu muda huo beki huyo alirejea kwao Togo, ambapo sasa Yanga wanataka kumrejesha kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kuelekea katika michuano ya kimataifa.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Chanzo kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Championi Jumatatu kuwa kiongozi huyo alienda Togo wiki iliyopita kwa ajili ya kuzungumza naye kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya ambao utamrejesha kwa mara nyingine beki huyo kwenye klabu hiyo.

“Kweli kuna kiongozi mmoja alienda kumfuata Bossou kule Togo kwa ajili ya kuzungumza naye kwa ajili ya kurejea tena kwetu, kwa sababu benchi la ufundi limeonyesha kumhitaji kwa ajili ya kuimarisha ulinzi zaidi. “Na tayari ameleta majibu kwamba yeye amekubali, kinachosubiriwa kwa sasa ni kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kisha yeye aje tumalizane naye, na hakuna ugumu juu yake kwa sababu kuna nafasi ya mchezaji mmoja wa kimataifa ipo wazi,” kilisema chanzo hicho.
Championi lilifanya jitihada za kumpata Bossou ambapo baada ya kupatikana, alifunguka: “Kweli Yanga wamekuja kuongea na mimi kwa ajili ya kunisajili, lakini nasikilizia wiki ijayo ndiyo nitajua kila kitu juu ya suala hilo. “Kwa sasa siwezi kuzungumzia sana lakini kila kitu kikikamilika ndipo nitazungumza, kwa sasa itambulike kama tetesi tu na kama unataka kujua zaidi ni bora ukawauliza viongozi wa Yanga na siyo mimi.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini