Kocha George Lwandamina ameuambia uongozi anahitaji mshambuliaji wa kati atakayefanya kazi yake kwa uafasaha zaidi.
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Novemva 15 na Lwandamina anataka kumaliza kazi mapemaaa.
Lwandamina tayari amewasilisha uamuzi wake kimyakimya na inaelezwa inatokana na kuendelea na ligi bila ya kuwa na mshambulizi wa kati kutokana na Donald Ngoma na Amissi Tambwe waliosajiliwa kwa nafasi hiyo kuwa majeruhi.
“Lwandamina anaona kama ataendelea hivyo, basi kutakuwa na tatizo.
“Anaona ligi inakwenda na bado Tambwe na Ngoma hawajawa vizuri na wakirejea hawawezi kuwa na mwendo mzuri itachukua muda.
“Pia inawezekana ana hofu huenda majeraha yao yasiwe na uhakika wa kupona kwa asilimia mia. Hivyo imekuwa ikitibua sana plani zake kwa kuwa Chirwa ni mzuri zaidi akitokea pembeni Tambwe au Ngoma wangekuwa fiti, Chirwa ndiye angechukua nafasi ya Msuva,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Pamoja na kuwakosa washambuliaji hao wawili, bado kocha huyo Mzambia amekuwa akijitahidi kuwatumia wachezaji wake wapya kama Raphael Daud na Pius Buswita kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini