Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mashabiki Yanga Wapagawa Wakodisha Basi Kwenda Kuwaona Ajib Na Tshishimbi


Mashabiki na wanachama wa Yanga Arusha wameamua kukodisha basi kubwa kwa ajili ya kwenda Singida kushuhudia mpambano baina ya mabingwa watetezi Yanga na timu ya mkoa huo kutokana na kutaka kuwaona ana kwa ana wachezaji Ibrahim Ajibu na Papy Kabamba ‘Tshishimbi’
Katibu wa Yanga, Arusha Destrich Kateule alisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kushindwa kwenda katika mikoa mingine kuiona timu yao inavyocheza badala yake wamekuwa wakiiangalia kwenye runinga pekee.
Alisema, “Arusha hatuna timu ya Ligi Kuu hivyo sisi kama wanachama na mashabiki wa Yanga tunakosa burudani ya kuwaona wachezaji wetu ana kwa ana, badala yake tunawaona kwenye runinga tu ambao wanaamua mchezaji wa kumuonesha.”

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017