Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Meli Kubwa Yenye Madaktari Bingwa Tayari Imewasili DSM


Meli kubwa ya Kisasa yenye Madaktari bingwa pamoja na wauguzi 381 iliyosheheni vifaa tiba pamoja na dawa imewasili jijini Dsm ikitokea nchini china kwa ajili ya kutoa huduma za Upimaji,upasuaji pamoja na tiba za aina yeyote bure ambapo wananchi wa Mkoa wa dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia kesho kujipatia matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akifuatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Madaktari kutoka katika hospitali mbali mbali za jiji la dsm walitembezwa katika meli hiyo katika maeneo tofauti ikiwemo vyumba maalum vya kufanyia upasuaji maeneo ya kufanyiwa vipimo vya hali ya juu-MRI pamoja na vyumba vya kulaza wagonjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda amewataka wananchi kutumia fursa ya Matibabu bure kujitokeza kuanzia kesho ili kupata vipimo,matibabu na dawa na hata Upasuaji wa aina yeyote bila gharama.

Aidha Makonda amewataka wananchi ambao wanasubiri kufanyiwa Upasuaji katika baadhi ya hospitali ambao bado wako katika foleni ya kupangiwa siku wafike katika meli hiyo na vyeti vyao ili wafanyiwe upasuaji,ambapo pia makonda alimshukuru balozi wa china aliyemaliza Muda wake kwa kutimiza ahadi ya kumletea madaktari wenye Utaalam na Vifaa vya hali ya Juu.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017