Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mbwa Wazua Taharuki Kwa Kula Mboga Iliyobandikwa Jikoni


Hali ni tete katika Mji wa Geita baada ya kuwepo ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurula mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji huo, baada ya mbwa hao kuanza kuvamia makazi ya watu kisha kukamata kuku pamoja na kula mboga iliyobandikwa jikoni kana kwamba hakuna mamlaka zinazohusika.

Mbwa hao wakiwa kwenye makundi makubwa wamevamia familia mbili za wakazi wa mtaa wa Nyanza katika Halmashauri ya mji wa Geita kisha kukamata na kuua kuku watano wa Bw,Benedict James kabla ya kuingia nyumbani kwa Bi,Mariam Agustino kisha  kula nyama kilo tatu iliyokuwa jikoni kwa maandalizi ya  mlo wa mchana hali iliyopelekea familia hiyo kushinda na njaa.

Akiongea kwa njia ya simu,Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya mji wa Geita  Abas Kilonge,mbali na kukiri kupokea malalamiko ya wakazi hao amesema kinachokwamisha zoezi la kuwapiga risasi mbwa hao ni fedha ila akadai mchakato wa  kupata fedha unaendelea.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017