Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mtanzania mwingine afuzu majaribio timu ya AFC ya Sweden


Kiungo mshambuliaji Rashid Chambo ,17, amefuzu kucheza kuitumikia timu ya AFC ya Sweden.

AFC ndiyo timu anayofanya majaribio Mtanzania, Said Hamis Ndemla.

Chambo kutoka JKT Ruvu alikwenda kufanya majaribio katika timu hiyo mwezi uliopita na sasa amefuzu.

Pamoja na kufuzu timu ya vijana, kocha amependekeza awe anapewa nafasi katika timu ya wakubwa.

“Kocha kaona ana kipaji, hivyo atakuwa akitumiwa pia na timu ya wakubwa. Lakini timu ya vijana inapokuwa na mechi, basi anakwenda kucheza,” kilieleza chanzo kutoka Sweden.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017