Haya ni maajabu na ni ngumu kuamini unaweza sema hivi, kutokana na Kanisa linalo tambulika kwa jina la Gabola limekuwa likibatiza watu kwa kutumia aina mbali mbali za pombe.
Kanisa hilo lipo nchini Afrika kusini ambapo linaongoza na mtu anaye jiita Askofu Tseitsi Makiti na ndiye muanzilishi wa Kanisa hilo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habarii kinasema Mtu huyo ameeleza anafanya hivyo na kuwakumbusha watu kwamba Yesu alibadili maji na kuwa waini hivyo watambue kuhusu hilo.
“Watu tunaokunywa pombe siku zote tuna furaha na amani hivyo hata watu wanaokuja kwangu kusali wanafuraha muda wote na wanafurahia huduma yangu” amesema
Amesema wamepokea watu kutoka kwenye jamii na wanaendelea kupokea ambapo watu wamekua wakifika kanisani hapo kubatizwa na kuapokea ibata na huku wakiendelea na utaratibu wao wa kunywa pombe.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini