Kuna taarifa amabazo siyo rasmi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa safari ya Kocha mkuu wa Yanga George LWANDAMINA kwenda Zambia kwenye Msiba ameenda kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kwenda kumalizana na timu yake ya zamani ZESCO.
YANGA leo kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten amesema Mwalimu George Lwandamina ameenda msibani Zambia na atarejea Jumatatu kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Mwalimu ameenda Zambia kwenye MSIBA na atarejea jumatatu, hilo la Zesco mimi siwezi kuzungumza maana mimi sipo ZESCO
Dismas Ten amesema pia Lwandamina bado anamkataba na Mabingwa hao wa Tanzania Yanga na kama masuala ya mitandaoni huwezi kuwazuia watu kuongea kwakuwa ndo sehemu ya Kuzungumza.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini