Kufuatia gazeti la Bingwa la November 13, 2017 kutoa taarifa ya Thomas Ulimwengu kutua Yanga wakati wa dirisha dogo na kusaini mkataba wa miezi sita wakati akijiweka sawa kabla ya kurudi kwenye soka la kiushindani barani ulaya Uongozi wa mchezaji Thomas Ulimwengu umetoa neno kuhusu Ishu hiyo.

Jamal Kisongo ambaye ndiye meneja wa Thom kwataunit.com tulimtafuta ili kutolea ufafanuzi suala hili naye hakusita kusema
Thomas anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi Januari na kwasasa yupo katika mapumziko na kwasasa anamkataba na klabu yake anawezaje kuja kujiweka sawa Yanga? Thomas hata angetaka kujiweka vizuri siyo Yanga na wala siyo timu za Afrika.
Jamal Kisongo msomaji wa Kwataunit.com amesema Thomas alishatoka Level za kucheza soka la Afrika hawezi tena kurudi kucheza Afrika kwasasa, kikubwa watu waelewe kuwa kuna vilabu vingi tu barani ulaya vinamwitaji hata angetaka kujiweka sawa angecheza katika vilabu nje ya Afrika.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini