Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Takukuru Yaanza Kulifanyia Kazi Suala la Nyalandu

Takukuru Yaanza Kulifanyia Kazi Suala la Nyalandu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), imesema kuwa suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema kuwa wakimkuta na hatia watamfikisha kunakostahili.

Kauli hiyo ya Mbugo ameitoa leo Jumanne ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala kumlipua Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 jana Jumatatu Dk Kigwangalla aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.

Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii. 

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017