Wakati dirisha dogo la usajili linafunguliwawiki ijayo,kuna habari kwamba Simba imepania kuwarejesha tena katika kikosi chao washambuliaji wake wawili,Daniel Lyanga na Elias Maguri wanaocheza soka nchini Oman.
Habari za uhakika ambazo zimetifikia zinaeleza kwamba Lyanga alikwenda katika klabu ya Fanja ya Oman kwa mkopo,na sio kwamba aliuzwa kama
ambavyo imekuwa ikidaiwa,na hivyo katika dirisha dogo anarejea kuendeleza makali yake.
Kwa upande wake Elias Maguri alisajiliwa na klabu ya Dhofar akitokea Stand United ya Shinyanga, lakini alitokea Simba kabla ya kuhamia katika klabu hiyo ya mkoani Shinyanga.
Simba inayoongoza Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara,imekuwa na makali katika safu ya ushambuliaji, lakini
inataka kuhakikisha inakuwa na washambuliaji wakali zaidi.
Mabao mengi ya Simba msimu huu yamefungwa na wachezaji wa nafasi ya
kiungo, na sasa kocha mkuu wa Simba Joseph Omog anataka kuhakikisha kwamba anakuwa na washambuliaji wanaofunga mabao.
“Kocha ameagiza kwamba anataka kuwa na washambuliaji wanaofunga,hana maana kwamba washambuliaji wa sasa katika Simba ni wabaya,lakini anataka kuhakikisha kwamba Simba inakuwa na washambuliaji ambao wanafunga mabao pia”amesema mmoja wa viongozi wa Simba.
Hata hivyo ameongeza kuwa Danny Lyanga hakuuzwa bali alitolewa kwa mkopo hivyo yeye ni mali ya simba.
“Sio kwamba Danny Lyanga aliuzwa kama watu wanavyofkiri, bali tulimpeleka kwa mkopo katika klabu ya Fanja ambayo ni klabu rafki wa Simba,baada ya viongozi wake kutuomba kwamba wanataka mshambuliaji mmoja akawasaidie kwa miezi sitatu” amesema.
Kuhusu Maguri, kiongozi huyo amesema kwamba wanataka kumrejesha baada ya kuridhika kwamba amekuwa katika kiwango
bora zaidi.
“Unajua Maguri aliondoka kwasababu ya kutofautiana mfumo na aliyekuwaKocha Mkuu wakati ule,Patrick Phiri, lakini bado anataka kuitumikia Simba”amesema na kuongeza kwamba mipango imeanza kuwarejesha wachezaji hao.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini