Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tetesi Za Usajili Yanga Leo Jumamosi Novemba 11 2017 Wanaoingia Na Wanaotemwa Hawa Hapa

Viongozi wa Yanga wamefika bei kwa mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Rashid aliyezaliwa mwaka 1995 wakati Tanzania ikifanya uchaguzi mkuu wa vyama vingi vya siasa.

Mpango wao ni kusajili mshambuliaji mmoja wa ndani na mwingine wa nje, sasa ndani upepo umeng'ang'ania kwa Mohammed ambaye Kocha George Lwandamina ameambiwa amuangalie kwa mara ya mwisho kwenye mechi dhidi ya Simba, Novemba 18 ndani ya Sokoine, Mbeya.

Mmoja wa viongozi mwenye ushawishi mkubwa ndani ya kamati ya usajili ya Yanga ameidokeza Mwanaspoti kuwa wao wanamkubali mchezaji huyo chipukizi na wamemuambia Kocha ajiridhishe kwenye mechi na Simba, akiwapa dole tu wanamaliza mchezo kwa gharama yoyote ile tena siku hiyohiyo.

Lwandamina ambaye anarejea nchini keshokutwa Jumatatu akitokea kwao alipokwenda kuhani msiba, atakutana pia na makali ya mchezaji huyo atakapoivaa Yanga Novemba 25 katika Uwanja wa Uhuru katika mechi ya ligi. Lakini huenda asifike kote huko kama mchakato wake ukimalizwa baada ya mechi na Simba.

"Hatutaki kumsajilia kocha kama ambavyo timu zingine zinavyofanya akisema hafai tutaanza kuangalia wale wa kigeni kutokana na hapa ndani hatudhani kama kutakuwa na kitu cha ziada tena kuzidi huyu wa Prisons,"alidokeza Kigogo huyo huku akitaka jina lake lisitokee gazetini kwasababu binafsi.

Lakini Mohammed ambaye huvaa jezi namba 10 ndani ya Prisons alipoulizwa na Mwanaspoti alisema; "Sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote kuhusu kujiunga na timu hizo kubwa kwa sasa kwani hakuna ambayo imenifuata."

"Kikubwa kwangu ni kuendelea kujituma na kufanya vizuri zaidi. Mnaweza kusema nitafunga zaidi kama nitakuwa nacheza sambamba na Ibrahim Ajibu, Emmanuel Okwi ama Shiza Kichuya lakini hilo linategemea, lengo langu ni kufunga angalau mabao 15 msimu huu," alieleza mchezaji huyo aliyefunga mabao sita kwenye mechi tisa.

"Siwezi kusema kama wakinifuata nitakwenda ama la, hilo kwa sasa lipo nje ya uwezo wangu, natazama zaidi kazi yangu,siwezi pia kusema kama timu yangu ya Prisons ikiniruhusu nitakubali kwenda, hapana, ni ngumu kuwa na jibu la moja kwa moja sasa," anafafanua mchezaji huyo ambaye si askari Jela.

Mzambia huyo alinukuliwa na Mwanaspoti akisema kwamba anataka uongozi wake kumtafutia washambuliaji wawili wenye makali zaidi ya Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wanaoibeba Yanga kwasasa.

Lakini habari za ndani zinadai kwamba kuna uwezekano Yanga ikafikiria kutengua mkataba wa mmoja kati ya Amissi Tambwe au Donald Ngoma ili kuingiza mashine moja ya kigeni.
source : Mwanaspoti

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017