Kuelekea dirisha dogo la Usajili VPL ambalo kesho November 15 litafunguliwa mpaka December 15 ambayo ndiyo itakuwa tarehe rasmi ya Kufungwa tayari tetesi mbalimbali zimeanza kutajwa, safari hii msomaji wa Kwataunit.com zikihusisha makinda wawili wa Yanga wanaotakiwa na timu ya Mbao ya jijini MWANZA.
Mbao ambayo inashiriki ligi Kuu ya soka nchini Tanzania VPL imewaandikia Yanga Barua ikiwa inawahitaji wachezaji Yusuph Mhilu na Edward Maka anayecheza nafasi ya Kiungo lakini kuna taarifa zinadai uongozi wa Klabu ya Yanga umeshindwa kuwapa majibu ya moja kwa moja uongozi wa Mbao ukisubiri majibu ya kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina kutoa majibu hayo kama anaweza akawaruhusu.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Android ===> Bofya hapa
Mhilu Na MAKA wametokea kwenye timu za vijana za Yanga wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga hivyo basi kuna taarifa kuwa wachezaji hao wanaweza wakatolewa kwa mkopo kwenda Mbao ili wapate nafasi zaidi ya kucheza.
Yanga inasemekana hawataki kuwaacha moja kwa moja wachezaji hao wenye asili ya Uyanga kutokana na wachezaji hao kupita timu za vijana hivyo basi wanaweza kutolewa kwa mkopo na kadiri wanavyokomaa ndipo watawarudisha Jangwani.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini