Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO:Rais Magufuli Akisikiliza Wimbo wa Kisukuma na Mama na Dada Yake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anasikiliza wimbo wa kabila la wasukuma pamoja na Mama yake mzazi, Suzana Magufuli na Dada yake Mkubwa Monica Joseph Magufuli.

Rais Dkt Magufuli yupo mapumzikoni kijijini kwake Lubambangwe, Chato Mkoani Geita.

Aidha, Rais anatarajia kufanya ziara Mkoani Kagera kuanzia tarehe 06 hadi 09 Novemba, 2017.

Dhumuni la ziara ya Mhe. Rais Magufuli ni kuwatembelea wananchi wa Mkoa wa Kagera pia kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani hapa.

Vilevile  Mhe. Rais Magufuli atapata fursa ya kuongea na wananchi  kwenye Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Ndege wa Bukoba. 

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017