Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Dereva Boda Boda akatwa sehemu za siri, Kisha Kuuawa

WATU wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti ndani ya wiki moja wilayani Geita mkoani Geita akiwemo mwendesha bodaboda na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ndize Gabriel (40) mkazi wa Mtaa wa Katoma mjini Geita aliyekatwa sehemu mbalimbali za mwili wake zikiwemo sehemu za siri huku wauaji hao wakitoweka nazo.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Latson Mponjoli, amesema tukio la kwanza limetokea Aprili 24 majira ya saa 12 alfajiri katika kitongoji cha Mzalendo, kijiji cha Ikina Kata ya Bukoli Geita baada ya watu wasiojulikana kumuuwa mlinzi Anderea Mnyambo(60)kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani wakati akilinda mgahawa wa Hussin Mayeye.

Amesema tukio la pili limetokea April 26 saa 9 asubuhi baada ya wananchi wenye hasira kali wakazi wa mtaa wa Kabaherere kata ya katoro Geita,kumuuwa kwa kumpiga na fimbo pamoja na mawe mtu mmoja ambaye hakufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28-30 wakati akitaka kupora pikipiki ya Emmanuel Mashiku (27) aliyekuwa amemkodi kumpeleka kijiji cha Inyala.

Kwa mjibu wa Kamanda Mponjoli, tukio la tatu ni la watu wasiojulikana kuumua kikatili mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ndize Gabriel(40)mkazi wa Mtaa wa Katoma mjini Geita kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake zikiwemo sehemu za siri na kutoweka nazo lililotokea Aprili 27, mwaka huu majira ya usiku.

Na kwamba, siku iliyofuata Aprili 28 katika poli la Kamhanga Wilayani Geita, mwili wa mwendesha bodaboda Mussa Mathayo mkazi wa Mbugani uliokotwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani huku wauaji wakiondoka na pikipiki aliyokuwa akiendesha yenye namba za usajili MC 918 AUY mali ya Hanifa Nuru.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017