Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Dr. Mwele Aeleza Vyombo Vya Habari Vilivyochangia Kutumbuliwa Na Rais Dkt Magufuli


Nafikiri changamoto kubwa ya vyombo vya habari nchini Tanzania ni ukosefu wa ujuzi miongoni mwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuwasilisha taarifa juu ya kazi za watafiti. Na wanaposhindwa kuwasilisha taarifa hizo kwa usahihi, sisi watafiti huwalaumu na ndio pale tunaamua kuwa tutakaa kimya kutozungumza na vyombo vya habari tena.
Hayo yalisemwa na Dr. Mwele Malecela wakati akifanya mahojiano na gazeti la The Citizen kuhusu maoni yake juu ya namna vyombo vya habari vinavyofanyakazi nchini Tanzania.
Dr. Mwele alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambapo uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dkt Magufuli Disemba 16 mwaka jana baada ya kile kilichodaiwa kuwa alitangaza kwamba Tanzania kuna ugonjwa wa ZIKA.
Kwa sasa kuna watu wengi nchini Tanzania wameamua kukaa kimya kutozungumza na vyombo vya habari kwa hofu kuwa kile watakachosema sicho kitakachowasilishwa kwa jamii.
Akizungumzia sakata la kuenguliwa kwake sababu ya taarifa zilizotolewa, Dr. Mwele alisema kuwa, tulikuwa katika mkutano ambapo tulijadili kuhusu magonjwa mbalimbali. Tulizungumza kuhusu Ebola, UKIMWI na mambo mengi mbalimbali, lakini waandishi wa habari wakaamua kuegemea kwenye suala la ZIKA pekee.
Alipoulizwa kuhusu madhara ya jambo hilo, alisema kuwa mwisho wa siku mtu alipoteza kazi yake.
Aidha, Dr. Mwele alisema kuwa licha ya hayo yote kutokea, hana mgogoro na wanadishi wa habari, lakini amependekeza kuwa kuwapo na waandishi wa habari wataalamu katika nyanja fulani, mfano sayansi, biashara, uchumi, siasa ambao ndio watakuwa wakiandika habari ili kuepusha matatizo zaidi.
Bila kuwapo na waandishi kama hao, itakuwa vigumu kwa watafiti kuendelea kufanyakazi na waandishi kwa hofu ya matatizo zaidi kutokea. Mwanzoni tulichukuliwa kuwa ni kawaida, sababu kazi ya mwandishi ni kuwasilisha ujumbe, basi haihitaji kuwa mtaalumu katika nyanja fulani ili aweze kuifanyia kazi, lakini sasa ni hatari kwani taarifa wanazozitoa kama si sahihi zinasababisha watu kupoteza kazi, na madhara mengine, alisema Dr. Mwele.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017