Baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la harufu mbaya mdomoni na maeneo mengine mwilini, kupasuka kwa kidomo, pamoja na kuumwa kichwa. Wengi wamekuwa wakihangaika kutafuta dawa ya kujitibu dhidi ya matatizo hayo bila kutaka kujua sababu ya kuwepo kwa matatizo yenyewe.
Wakati mwingine mwili hutoa dalili fulani ili kuashiria kuwa umepungukiwa na vitamini au baadhi ya madini muhimu. Utafiti uliofanywa na ‘Healthspan’ umeonyesha kuwa watu 6 kati ya 10 hawajui chochote kuhusu kuzibaini dalili hizoo zinazotolewa na mwili.
Dalili nyingine ambazo mwili huzionyesha kutokana na upungufu wa madini ya muhimu au kutokuwa na lishe iliyo bora ni pamoja na kuwa na nywele nyepesi, alama nyeupe katika kucha, mba, pamoja na ngozi kavu.
Lakini kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe kutoka London, Rob Hobson, kuongeza mboga mboga, nyama nyekundu na karanga katika mlo wako inaweza kusaidia kupambana na dalili hizo.
Hizi hapa ni baadhi ya dalili zinazotolewa na mwili na vyakula unavyoweza kuvitumia ili kupambana nazo.
Midomo kupasuka
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa madini ya chuma au vitamini C
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: Nyama nyekundu, pilipili, mboga aina ya spinach pamoja na samli.
Mba
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa vitamini B7, vitamini H na upungufu wa mafuta ya asidi.
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: Siagi ya karanga, mbegu za alizeti, samaki wabichi pamoja na lozi.
Kukauka kwa ngozi
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa Omega-3
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: mbegu za alizeti, karanga na mbegu za ufuta
Chunusi
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa madini ya Zinki
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: mchicha, korosho na unga wa kakao
Harufu mbaya mdomoni
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa madini ya Chuma
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: Zabibu, mbaazi, kifungua kinywa cha nafaka pamoja na maharage ya adzuki
Pua kuwa na mafuta mengi
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa vitamini B2 au madini ya Zinki
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: Parachichi na lozi.
Kichwa kuuma
Inaweza kuwa dalili ya: Upungufu wa vitamin B12, B6 na madini ya Magnesium
Vyakula vinavyoweza kukusaidia kupambana na hali hiyo: Mbegu za maboga, maziwa ya soya pamoja na ndizi mbivu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini