Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Flora Mbasha Amtaja Mwanaume Atakayefunga Nae Ndoa Wiki Ijayo


MWIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini, Madame Flora (Flora Mbasha zamani), Jumapili ya wiki ijayo anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza.
Madame Flora ameliambia Swaggaz kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa Wakati Wake pamoja na kitabu alichokipachika jina la Siri za Flora Mbasha.
“Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu, watu wote wanakaribishwa kadi zimebaki chache tu kutokana na idadi ya ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora.
Awali. Flora alikuwa ameolewa na mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha lakini walitengana.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017