Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Usalama Wa Watoto Wa Rais Mugabe Upo Hatarini, Wahamishwa Nchi


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe imearifiwa kuwa amewahamishia watoto wake wawili nchini Afrika Kusini kufuatia usalama wao kuwa mashakani.
Watoto hao wawili, Robert Jr na Bellarmine Chatunga wamehamishiwa nchini humo ambapo mmoja alitokea Dubai na mwingine Zimbabwe na sasa wanaendelea na masomo jijini Johannesburg.
Robert Jr aliondolewa kutoka Dubai kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa, huku Bellarmine akiondolewa Zimbabwe ili aweze kutilia mkazo masomo yake akiwa mbali na familia hiyo ambayo kwa siku za karibuni imekuwa na mivutano ya kisiasa ambayo ingeweza kumfanya asisome vizuri.
Sababu kubwa imeelezwa kuwa ni suala la usalama wao ambapo wangeweza kuwa walengwa na kujikuta kwenye matatizo hasa yatokanayo na siasa za nchi hiyo. Hivyo kuwaweka mbali na familia hiyo kunawasaidia wasiwe waathirika wa kisiasa kwa hali ya uongozi nchini humo si salama.
Mwaka jana, Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe aliibua madai kuwa, wanajeshi na viongozi wengine wa chama tawala, ZANU-PF ambao wanatamani madaraka, walitaka kumuua mwanae Chatunga.
Afrika Kusini imekua ni nchi ya makazi ya raia wengi walioikimbia Zimbabwe kutokana na uongozi wa Mugabe na kuzidi kudorora kwa uchumi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017