Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mtanzania Alphonce Simbu Ameshika Nafasi ya 5 London Marathon

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Simbu.
Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Simbu, leo Jumapili amefanikiwa kushika nafasi ya tano katika mashindano ya mchezo wa riadha ya mbio ndefu jijini London (London Marathon).
Simbu ameshika nafasi hiyo baada ya kutumia muda wa saa 2:09:10 wakati mshindi wa kwanza Daniel Wanjiru, 24, wa Kenya alitumia saa 2:05:56 akifuatiwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia aliyezidiwa kwa sekunde 5 tu.
Washindi wa tatu na wanne wote ni Wakenya ambao ni Bedan Karoki (2:07:41) na Abel Kirui (2:07:45).



Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017