Msanii wa hip hop nchini Tanzania Nikk Wa Pili amesema kuwa mastaa wengi wa Bongo Movie tunawafahamu sana kuliko kazi zao tofauti ilivyo kwa wasanii wa filamu za nje.
Nikk Wa pili alizungumza hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) nakusisitiza kuwa mastaa wengi wa bongo wanatrendi kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka mitatu (3) kwa mambo mengine lakini movie zao hazijulikanii kabisa.
"Ni kweli mastaa wengi wa movie Tanzania tunawafahamu sana wao kuliko kazi zao, kuna mtu unamsikia na unamuona anatrendi kwa miaka mitatu lakini hauijui movie yake hata moja" alisema Nikk Wa Pili.
Nikk ametoa mfano wa kupitia msanii maarufu wa Bongo Movie nchini Ray Kigosi na kusema hafahamu movie yake hata moja lakini ishu yake kama ile ya kuywa maji sana aliisikia na ilitrendi kweli kweli.
"Sizifahamu movie za Ray Kigosi lakini ishu yake ya maji naijua, ile ishu kwamba anakunywa sana maji niliisikia sana lakini movie zake sizijui" - alisisitiza Nikk Wa Pili.
Mbali na hilo Niki wa Pili alisema yeye anaona kwenye tasnia ya filamu kuna changamoto hivyo wasanii wa bongo movie wanapaswa kujitafakari, huku akiwashukuru sana wasanii hao kuisaida bongo fleva kufanya vizuri, huku akiwashauri kuwa wakitumia nguvu hiyo hiyo wanayoitumia kupush muziki wa bongo fleva inaweza kusaidia sana kazi zao za sanaa wakuwafikia watu na watu kuzijua kazi zao zaidi kuliko kujua matukio yao.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini