Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

ZIMBABWE: Mtoto Aliyeamua Kumuoa Mama Yake Amuacha Baada ya Kuambiwa Mama Yake Amemlisha Limbwata.


Kijana mmoja nchini Zimbabwe kwa jina la Farai aliefunga ndoa na mama yake mzazi, ameamua kuachana nae baada ya kugundua mama yake huyo (mke) kutumia nguvu za giza na kwenye chakula hili kijana wake avutike na penzi la mama yake mzazi.

Kijana huyo anasema mama yake (mke) alikuwa hataki mwanawe (mume) ale chakula sehemu nyingine yoyote zaidi ya chakula cha nyumbani kwao, sasa hapo kwa mujibu ya Farai ndio alikuwa anamnyunyuzia limbwata au ndumba, kijana huyo akaenda Afrika ya Kusini kwa Pastor Mbolo akamuombea.

Baada ya kuombewa na Pastor Mbolo bwana mdogo Farai akaanguka chini akiwa amefumba macho na kutapika vitu visivyoeleweka vikidhaniwa ni limbwata alilokuwa anawekewa kwenye chakula na mama yake mzazi.

Ndugu Farai hataki tena kumuona mama yake (mke) na simu amekata mawasiliano nae na yeye mwenyewe anashangaa kumuoa mama yake mzazi wakati ikiwa wasichana wa umri wake wapo.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017