Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO: CUF ya Maalim Seif Yaamua Kumvagaa Lipumba Buguruni

 Leo APRILI 27, 2017, wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama hicho  Maalim Seif Sharif Hammad wamesema kuwa Jumapili hii wataandamana hadi Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam kwa ajili kwenda kufanya usafi kwenye ofisi hizo.
Wakizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma, wafuasi hao wameeleza kuwa, japokuwa ofisi hizo anazikalia Prof. Ibrahim Lipumba ambaye wanadai kuwa siye Mwenyekiti halali wa CUF.
Aidha wameeleza kuwa lengo lao ni kufanya usafi na si kufanya vurugu kama wengi wanavyodhani, hivyo usafi huo utakuwa maalum kwa ajili ya kuandaa mazingira safi ya Katibu Mkuu wao kwenda kufanya kazi zake vyema kwenye ofisi iliyo safi.
WASIKIE WAFUASI HAO WAKIZUNGUMZA

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017