Siku chache baada ya mastaa wa Bongo movie kuandamana hadi Kariakoo wakitaka filamu za kigeni zizuiliwe nchini, kumeibuka hoja mbalimbali huku watu wengi wakioneshwa kutofurahia uamuzi huo. Mastaa hao wa Bongo movie wakiongozwa na staa wa muda mrefu Jacob Stephen ‘JB’ wamedai kuwa kufanya hivyo ni kutokana na ukweli kwamba wanataka kuzipa nafasi zaidi filamu za Tanzania. Kutokaka na kukosolewa kwa kitendo hicho na wadau mbalimbali nchini JB ametumia account yake ya Instagram kutoa ufafanuzi zaidi ambapo moja ya mambo aliyoyagusia ni kuwataka watu kutohusisha kila kitu na siasa akisema pia kuwa kwenye shida hatojali nani anamsaidia alimradi anagusa maslahi yake. Bonyeza play kutazama hapa chini…
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka