Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO:Mashuhuda Wasimulia Tetemeko Lilivyotokea Kagera Usiku Wa Kuamkia Leo

picha kutoka maktaba

Tetemeko la ardhi limetokea tena mkoani Kagera na kusababisha hofu kwa wananchi.
Hofu hiyo inatokana na tetemeko la ukubwa wa 5.7 kwa vipimo vya Richter lililotokea mkoani hapa Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 majeruhi takriban 200 na mamia wengine kukosa makazi.
Wananchi waliozungumza nasi, katika Manispaa ya Bukoba, wilaya za Missenyi, Muleba na Karagwe wamesema tetemeko hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wananchi mjini Bukoba walilazimika kulala nje ya makazi yao kutokana na kishindo cha tetemeko hilo.
Video yote nimekuwekea hapa chini ruksa kuitazama…


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017