Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Wolper Acharukia Wasanii Wenzake Asema Wengi Ni Wanafiki

Staa mwenye kiwango cha juu Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe.
Staa mwenye kiwango cha juu Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe amefunguka kuwa, wasanii wengi waliopo kwenye tasnia ya filamu ni wanafiki na wanafuata mkumbo, hawako kiuhalisia.

Akizungumza na Showbiz, wakati wa maandamano ya kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji na uuzwaji holela wa sinema za nje, Wolper alisema kuwa, wasanii wangekuwa na umoja wangeungana siku hiyo kwa ajili ya kujua hatima ya kazi zao wanazozifanya na zinazowaweka mjini, lakini kwa kuwa wengi ni wanafiki imeshindikana.
“Nachukizwa na unafiki Bongo Movi, kwa kweli unakera sana, hawako kiualisia ndiyo maana kufika tunapotaka ni ngumu sana,” alisema Wolper.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017