Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

AIBU:Baby Madaha Adaiwa Kuhongwa Gari Na Kisha Kupokonywa

MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amegandwa na skendo ya kuhongwa gari kisha baadaye kupokonywa na aliyekuwa meneja wake, Joe Kairuki, Ijumaa limevujishiwa hii ‘untold story’.

Ilidaiwa kuwa, kipindi cha nyuma wakati Madaha akiwa Kenya chini ya Lebo ya Candy ‘n’ Candy ya Joe, wawili hao walianzisha uhusiano wa kimapenzi ndipo mwanadada huyo akapewa ndinga hiyo aina ya Audi ya kuuzia sura.
Baada ya Madaha kupewa gari hilo, alijinadi kuwa, amepewa ikiwa ni sehemu ya mkataba wake lakini wanaoujua mchezo mzima wakavujisha ubuyu kuwa, alihongwa na baadaye akapokonywa.

Baby Madaha
Katika kuashiria kuwa madai ya kuhongwa yana ukweli f’lani ndani yake, baada ya Madaha kuachana na jamaa huyo, gari nayo akapokonywa na aliporudi Dar hakuwa na usafiri. Kufuatia madai hayo kusambaa kwa muda mrefu, hivi karibuni gazeti hili lilizungumza na Madaha na alipobanwa kuwa lile gari halikuwa lake bali alihongwa kisha akapokonywa alisema: “Hao wanaosema nilihongwa wana ushahidi gani? Ile gari nilipewa kama sehemu ya mkataba wangu, nilipomalizana nao nikaona nisije nayo Dar, nikaiuza.
Ijumaa: Ubuyu uliopo ni kwamba, Joe alikuwa mpenzi wako ndiyo maana akakupa ile gari, mlivyozinguana akachukua gari yake.

Madaha: Kwanza Joe hakuwahi kuwa mpenzi wangu jamani.
Ijumaa: Sasa wewe unasema uliiuza, mbona inadaiwa Joe ndiye anayeitumia kwa sasa?
Madaha: Niliyemuuzia ni rafiki yake aliyekuwa Mombasa, sasa kama imemrudia tena sijui imekuwaje.
-GPL

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017