Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

AIBU:Mchungaji Akamatwa Baada Ya Kuoa Mke Wa Muumini Wake


Mchungaji wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe, Jafece Josephat anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa mke wa muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai ameoteshwa na Mungu.

Mchungaji huyo amekamatwa leo baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.


Mheruka alitoa agizo la kukamatwa kwa mchungaji huyo kutokana na baba wa Appolo aliyenyanganywa mke kujitokeza mbele ya kanisa hilo na kudai mahari aliyomtolea mtoto wake irudishwe kwani hawezi kuutolea mahari ukoo mwingine kwa kuwa mke ameshaolewa na mme mwingine.



"Kwa kuwa, mke ameacha familia yake akaja kuolewa na wewe mchungaji amezini na kwa kuwa wewe unayejiita mchungaji umeiacha familia yako ya watoto watano ukaoa mke mwingine nyote mnazini kwani kinachotenganisha ndoa ya mke na mme ni kifo lakini nyie mmejichukulia maamuzi yenu binafsi,"amesema Mheruka.
Mheruka amemwagiza mwangalizi wa kanisa hilo kuendelea kutoa huduma katika kanisa hilo ndani ya miezi sita huku akitafuta utaratibu wa mchungaji mwingine mwenye maadili mema na kuwa wao kama Serikali watachunguza vizuri kama kanisa hilo limesajiliwa au halijasajiliwa ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017