Pilipili kichaa inaweza kustawi sehemu mbalimbali na inahitaji siku 100 za
ukuwaji.Hustawi zaidi kwenye mazingira ya joto na unyevunyevu.Mmea huu hukua
kufikia urefu wa futi mbili hadi nne.Ina wingi wa vitamini A,pia ina vitamini
B,vitamini E,vitamini C,Riboflavin,Potassium na Manganese.
- Jamii nyingi hususa
Marekani na bara la Asia wana historia ya kutumia pilipili kichaa kama tiba.Ni
dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi,hutumika sana kwa kusafisha damu na
kutoa sumu mwilini,pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano
wa tindikali(acid)mwilini.Pilipili kichaa imetumika kwa maradhi tofautitofauti
ikiwemo moyo,gauts,kupooza,homa,kikohozi,tonsilatis,kichefuchefu na hemorhoids
kwa miaka mingi huko Asia na mashariki ya mbali.
MAAJABU YA PILIPILI
KICHAA;
1.Kutibu
kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba
liyothibitishwa na imekuwa ikitumika miaka kadhaa iliyopita katika nchi mbalimbali.Sio
tu kuzuia kutokwa na damu katika kidonda cha kujikata kama ilivyozoea kutumiwa
na wengi huko majumbani kwa miaka mingi bali pia huzuia fangasi na bakteria
kuingia katika uwazi wa kidonda hicho hutumika pia kuondoa sumu mwilini
2.Hufanya
mwili kuweza kutumia vyema virutubisho vipatikanavyo kutokana na chakula
3.Husaidia
uyeyushaji wa mafuta mwilini/Kuchoma mafuta
4.Pilipili ina
antioxidants muhimu kama beta carotene,ina wingi wa vitamini A,C na K hebu
tuziangalie vitamini hizo:
a.Vitamini A
husaidia kuweka sawa kinga ya mwili pia hutukinga na kansa na magonjwa ya moyo
b.Kazi ya vitamini C-ni kuzuia strock,magonjwa ya moyo,macho na kansa mbalimbali.Miili ya binadamu haiwezi kujitengenezea vitamini C,hivyo basi tunaweza kupata vitamini C kupitia chakula.
c.Vitamini K-Husaidia katika ukuwaji wa mifupa,pia ni muhimu katika mzunguko wa damu.Pilipili zote huwa na Capsaicin ambayo kazi yake ni kupunguza maumivu,kuzuia kansa na magonjwa ya moyo.
5.Inasaidia sana
kusawazisha sukari kwenye damu
6.Huwasaidia watu
wanene(over weight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari.Hii ni kwa mujibu wa
watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania uliochapishwa katika American Joarnal
of Clinical Neutition mwezi julai 2006.
7.Inasaidia kwa
kiasi kikubwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa INSULIN kwa 60% baada ya kula chakula
8.Husaidia
kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa RHEMATOID na
ARTHRITIS kupata nafuu
9.Husaidia kuondoa
mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini
10.Husaidia
kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue
kwa urahisi.
11.Husaidia
kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.
12.Husaidia
kuongezeka kiwango cha METABOLIC ambayo husaidia kuchoma mafuta
13.Husaidia
kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu.
14.Husaidia
kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini