Mwigizaji Faiza Ally ameleza jinsi mahusaino ya kimapenzi yalivyokuwa yanamsumbua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hali iliyopelekea yeye kuugua mara kwa mara
Faiza Ally na Sugu
Kupitia instagram Faiza amepost picha akiwa kitandani na kuandika, ‘‘Kuna mambo sasa hivi nikiangalia nacheka sana … haya mapenzi jamani, hapo ni miaka mitatu iliyopita nilikuaga namlilia Baba Sasha mpaka natundikiwa drip halafu narusha Facebook picha ili anione labda atanihurumia au tu ataniuliza unaendeleaje nimsikie tu lakini wapi inakua holaaaaa.
Picha aliyopost
“Pamoja na yote sijawahigi kujuta kumpenda na sijawahi kuacha kumpenda #throwback about 3 years ago…. asante facebook kwa kumbukumbu ambazo kwa wakati huo ilikua ni uchungu lakini kwa sasa imekuwa nikichekesho kwangu, simcheki mtu akililia mapenzi yake maana najua vile ana feel … mapenzi ya kweli hayafi,” aliandika Faiza.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini




