Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Hemed: JPM Kanishikisha Adabu ya Pesa

Tozi mwenye makeke katika tasnia ya filamu Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’.
TOZI mwenye makeke katika tasnia ya filamu Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amekiri kubadili mfumo wa matumizi yake ya fedha, ambapo amekuwa na nidhamu ya hali ya juu kufuatia ugumu wa upatikanaji wa pesa uliopo kwa sasa.

Akichonga na Star Mix, Hemed alisema zamani alikuwa na matumizi mabaya ya pesa, ambapo aliweza kutumia zaidi ya shilingi lakini tatu kwa siku, kwani alikuwa na njia na mbinu nyingi za kupata zingine, tofauti na sasa.

“Uchumi umebadilika, nimekuwa na nidhamu sana ya matumizi yangu, namshukuru Rais John Magufuli kwa kutuwekea mfumo mzuri wa kufanya kazi na kupata kipato kwa uhalali na si ujanjaujanja, nimekoma na nimenyooka, kwa sasa nimeweza kufanya mambo ya msingi na si starehe kama nilivyozoea,” alisema Hemed.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017