Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Inaumiza Sana Kuona Yanayoendelea Mtandaoni Kuhusu Zari Na Kifo Cha Ivan

UKWELI WATANZANIA MITANDAO IMETUPELEKA MBALI NA KUSAHAU HATA UTU WETU NA KUFIKIA HATUA YA KUONA MAISHA YA MTANDAO NDIO KILA KITU.PIA INAWEZEKANA WENGI WETU KWA KUWA MAISHA YANAYOENDELEA WATU HAWAYAJUI NDIO MANA INAKUWA RAHISI KWETU KUWANYOSHEA VIDOLE WALE AMBAO MAISHA YAO YAKO WAZI ILA TUSIJISAHAU HATA KAMA MAISHA YAKO NI YA SIRI MUNGU ANAWEZA KUKUFICHUA.A

Najaribu kwa muda kuuvaa u zari nione anapoingia mitandaoni anayokutana nayo anajisikiaje ila naona ni mazito kwake sema hawezi yazungumza.Ila kinachoumiza zaidi ni pale ambapo hata mwili wa marehemu haujazikwa wa Tanzania tushaanza kuitawala mitandao kwa msiba huu kama vile sisi ni waganda au watu wa afrika kusini.Yani mtu sasa hivi anakaa anawaza atunge uongo gani auandike kuhusu @zarithebosslady na familia yake ili page yake ipate uhai mwisho wa siku mtu anaandika vitu ambavyo ukisoma unaweza hisi ni shetani ameandika ujumbe ule na sio binadamu.

Ila eti ukiwauliza watu wanaofanya hivyo utakuta chuki zao zimeanzia pale ambapo @zarithebosslady aliingia kwenye mahusiano na @diamondplatnumz sasa ndio unakuta mtu bado anatumia kumchafua kwenye msiba huu kama njia ya kulipiza.

Kinachonisikitisha zaidi hata yule ambaye wa Tanzania wamemuamini kuwa mtetezi wa haki za watu @mangekimambi_ leo naye anasimama na kuandika vitu vya kupotosha watu tena kipindi hiki cha msiba na at the same time ukiuliza kwanini anafanya hivyo ni muunganiko wa chuki zile zile za diamond kuwa na zari ndio inapelekea mtu kukosa utu.

This is sad very sad kwa wa Tanzania leo @ivandon aliyekuwa na mali nyingi amefariki leo wewe ambaye una hako kasimu kako ka kuingia insta unajisahau na kushadadia misiba kama utaishi milele aisee.

Nadhani ingekuwa busara sana watu wakaacha familia ikamaliza mambo yao mana nahisi pia hizi page zinazozusha ujinga soon baada ya msiba zitadhalilika maana yale wanayopigia kelele kumzalilisha zari yatamalizwa kifamilia.
IFIKE HATUA TUJITAMBUE KUWA SWALA LA MSIBA LINAWEZA KUMPATA KILA MTU NA MATATIZO YA KIFAMILIA YANAMPATA KILA MTU .

HII NI MITANDAO TU ISIKUTOE UFAHAMU SABABU YA USHABIKI MAANDAZI WA TEAM KUMBUKA UTU WAKO.. UJUMBE KUTOKA KWA 
-blog ya wananchi

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017