Serikali kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma yatoa taarifa ya utekelezaji wa matokeo ya uhakiki wa vyeti feki, waliojinufaisha na zoezi pamoja na ajira mpya. Katika swala la vyeti feki inasemekana kuna watu pia walikwenda baraza la mitihani na kutaka kutoa rushwa ya Shilingi milioni Mbili na wengine Milioni tatu ili taarifa za vyeti vyao vibadilishwe. Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma imetoa taarifa pia kuhusu hilo na kudai kuwa wamefatilia na majina ya wahusika wanayo.
Pia imetangaza nafasi za kazi 15,000 za watumishi wa umma kwa kada mbalimbali ambao wataajiriwa kuanzia 03 Mei 2017. Pia waajiriwa wote kabla ya kuajiriwa lazima vyeti vyao vya elimu na utaalamu lazima vihakikiwe na mamlaka husika kabla ya kuajiriwa. Taarifa kamili Hii Hapa
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini