Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wao waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi amewaachia huru leo wabunge hao baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Hakimu Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani alimjeruhi.
Ushahidi wake ulielezea jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.
Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema;
“Sijui alishikwa matiti na nani?”
Kutokana na ushahidi huo Hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini