Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Madereva 6 Wa Halmashauri Walioghushi Vyeti, Wahukumiwa Mwaka Moja

Madereva sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wamehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kughushi vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira.

Hukumu hiyo imetolewa leo  na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kilwa, Gabriel Ngaeje baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani.

Madereva waliohukumiwa ni Juma  Sungura, Issa Abdurahman, Abdul Chubi, Dactuce Joseph, Ahmad Selemani na Abdallah Kilolopera.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017