Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kesi Ya Unga..Manji Atii Agizo La Mahakama Kuu ya Kisutu

Wakati kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara maarufu nchini, Yussuph Manji imeahirishwa hadi Juni 23, 2017, mfanyabiashara huyo ametii agizo la mahakama lililomtaka awe anahudhuria katika kesi yake.
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha ameiahirisha kesi hiyo mara baada ya Wakili wa Serikali, Adolf Mkinii kudai upelelezi bado haujakamilika.

Manji alikuwepo Mahakamani leo kwani mara ya mwisho aliagizwa awe anafika.
Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 ambapo anadaiwa kuwa, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017