Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mahakama Yakwama Kutoa Uamuzi Kesi ya Wema Sepetu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kutoa uamuzi wa ama kupokea au kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu Hakimu hajamaliza kuandaa uamuzi huo.

Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November 1, 2017.

Awali, Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba Mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.

Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017